Psalms 145

Wimbo Wa Kusifu Ukuu Na Wema Wa Mungu

Wimbo wa Sifa. Wa Daudi.

1 aNitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme,
nitalisifu jina lako milele na milele.
2 bKila siku nitakusifu
na kulitukuza jina lako milele na milele.

3 c Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana,
ukuu wake haupimiki.
4 dKizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine,
watasimulia matendo yako makuu.
5 eWatasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako,
nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu.
6 fWatasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha,
nami nitatangaza matendo yako makuu.
7 gWataadhimisha wema wako mwingi,
na wataimba kwa shangwe juu ya haki yako.

8 h Bwana ni mwenye neema na mwingi wa huruma,
si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo.
9 i Bwana ni mwema kwa wote,
ana huruma kwa vyote alivyovifanya.
10 jEe Bwana, vyote ulivyovifanya vitakusifu,
watakatifu wako watakutukuza.
11Watasimulia utukufu wa ufalme wako
na kusema juu ya ukuu wako,
12 kili watu wote wajue matendo yako makuu
na utukufu wa fahari ya ufalme wako.
13 lUfalme wako ni ufalme wa milele,
mamlaka yako hudumu vizazi vyote.

Bwana ni mwaminifu kwa ahadi zake zote
na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.
14 m Bwana huwategemeza wote waangukao,
na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao.
15 nMacho yao wote yanakutazama wewe,
nawe huwapa chakula chao wakati wake.
16 oWaufumbua mkono wako,
watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai.

17 p Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote,
na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.
18 q Bwana yu karibu na wote wamwitao,
karibu na wote wamwitao kwa uaminifu.
19 rHuwatimizia wamchao matakwa yao,
husikia kilio chao na kuwaokoa.
20 s Bwana huwalinda wote wampendao,
bali waovu wote atawaangamiza.

21 tKinywa changu kitazinena sifa za Bwana.
Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu
milele na milele.
Copyright information for SwhNEN